AFGHANISTAN- INDIA-SHAMBULIO

Afghanistan: shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa India

Vikosi vya usalam vya Afghanistan wakati wa mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Mazar-i-Sharif, Afghanistan, Aprili 9, 2015.
Vikosi vya usalam vya Afghanistan wakati wa mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Mazar-i-Sharif, Afghanistan, Aprili 9, 2015. AFP/AFP/

Watu wenye silaha wamejaribu Jumapili hii jioni kuteka Ubalozi wa India katika mji wa Mazar-i-Sharif, kaskazini mwa Afghanistan, wakati ambapo Waziri mkuu wa India akiiunga mkono serikali ya Kabul lakini pia mpinzani wake Pakistan.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya dhidi ya maslahi ya India nchini Afghanistan, ambayo hadi jioni yalikua hayajadaiwa na kundi lolote, yameambatana na mashambulizi mengine, yalioemndeshwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu dhidi ya kambi muhimu ya Pathankot, katika jimbo la Punjab.

Katika mji wa Mazar-i-Sharif, kwenye umbali wa kilomita 300 kaskazini magharibi mwa mji wa Kabul, milipuko miwili imesikika saa 10:30 saa za kimataifa Jumapili hii, kwa mujibu wa mwandishi wa shirika la habari la Ufaransa AFP ambaye ametembelea eneo hilo, kisha milio ya risasi imesikika.

"Tumeshambuliwa, na milio ya risasi inaendelea kusikika", mwanadiplomasia mmoja wa India ambaye alikimbilia katika eneo salama la jengo lilio jirani na ubalozi huo amesema, alipohojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP.

"Mashambulizi haya dhidi ya ubalozi mdogo wa India. Hatujui kama wapiganaji wameweza kuingia ndani", amesema Munir Farhad, msemaji wa mkuu wa jimbo la Balkh, ambapo Mazar-i-Sharif ni mji wake mkuu. Kwa mujibu wa kiongozi huyo vikosi vya usalama vimelizingira eneo hilo, ikiwa ni pamoja na jengo.

Vikas Swarup, msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya India, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba hawajapata taarifa yoyote kuhusu hasara iliyotokea katika shambulio hilo.