SRI LANKA-MARIDHIANO

Sri Lanka yaahidi kutoa ardhi kwa waathirika 100,000 wa vita

Rais wa Sri Lanka, Maithripala Sirisena, wakati wa mahojiano na shirika la habari la Ufaransa AFP, Januari 3, 2016, Colombo.
Rais wa Sri Lanka, Maithripala Sirisena, wakati wa mahojiano na shirika la habari la Ufaransa AFP, Januari 3, 2016, Colombo. AFP/AFP

Hadi wakimbizi wa ndani 100,000 nchini Sri Lanka ambao bado wanaishi katika makambi, miaka sita baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, watapewa sehemu za ardhi ili waweze kujenga nyumba zao, rais Maithripala Sirisena amesema katika mahojiano na shirika la habari la Ufaransa AFP.

Matangazo ya kibiashara

"Ni idadi kubwa, lakini nitahakikisha kwamba watu wote waliokimbia katika kisiwa cha Etat kusini mashariki mwa India katika Bahari ya Hind, wanapata sehemu za ardhi ili waweze kujenga nyumba zao", rais Maithripata Sirisena amesema.

"Ninaweka utaratibu wa kukamilisha mpango ndani ya miezi sita ijayo", rais Maithripala Sirisena ameongeza.

Baada ya kuchaguliwa mwezi Januari 2015, rais wa Sri Lanka amekua akipongezwa na jumuiya ya kimataifa kwa jitihada zake za kurejesha sehemu za ardhi, baada ya moja ya machafuko yaliyochukua muda mrefu na kusababisha maafa makubwa barani Asia: waasi wa Tamil Tiger waliangamizwa mwaka 2009, baada ya miaka 37 ya mapambano ya kujitenga.

Lakini shinikizo la kimataifa pia linamkabili rais huyo ili aweze kuongeza kasi ya maridhiano katika nchi hiyo ambayo imegawanyika kikabila.

Rais Maithripala Sirisena ameliambia shirika la haabri la Ufaransa AFP kwamba serikali iko tayari kutoa sehemu za ardhi kwa wakimbizi wa vita katika majimbo ya Kaskazini na Mashariki, lakini pia katika jimbo la pwani la Puttalam, kaskazini magharibi, katika miezi sita ijayo.

Katika jimbo la Jaffna (kaskazini), eneo ambalo lilishuhudiwa mapigano makali, rais wa Sri Lanka alitembelea mwezi uliopita kambi ya wakimbizi wa ndani ambapo familia 1,300 zinaishi kwa miaka 25 sasa.

"Hali hii haikubaliki. Nataka kumaliza tatizo hili mara moja na kwa wote. Kwa watu wengi, suala kubwa ilikua ukosefu wa ardhi. Tutalitatua", rais Maithripala Sirisena ameongeza.

Hata hivyo rais pia anataka kutoa katika wiki ijayo ardhi binafsi zilizochukua na jeshi, hasa katika maeneo ya zamani ya vita, kaskazini na mashariki mwa Sri Lanka.