CHINA-KUMBUKUMBU

Sanamu kubwa ya Mao yajengwa China

Sanamu kubwa ya Mao Tse-tung, lililopigwa picha Januari 4, 2016 katika mkoa wa Hunan, katikati mwa China.
Sanamu kubwa ya Mao Tse-tung, lililopigwa picha Januari 4, 2016 katika mkoa wa Hunan, katikati mwa China. AFP/AFP

Sanamu ya mita 37 ya Mao Tse-tung imejengwa katika mkoa wa Hunan, katikati mwa China, kwa mujibu wa mtandao wa habari wa China, hali ambayo imezua hali ya sintofahamu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa gharama ya Yuan milioni tatu (sawa na Euro 420,000) zilizofadhiliwa na kundi la wajasiriamali wa mkoa huo, kwa mujibu wa mtandao wa HMR.cn, sanamu ya dhahabu, iliyowekwa katika shamba, inamuonyesha kiongozi wa zamani wa kikomunisti akiketi juu ya kiti, akitafakari, mikono ikikunjwa.

Ujenzi wa sanamu hiyo ulimalizika mwezi Desemba baada ya miezi tisa ya kazi hiyo, kwa mujibu wa mtandao huu.

Licha ya mamilioni ya vifo ambavyo anatuhumiwa muasisi wa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949, Mao, ambaye alifariki dunia mwaka 1976, bado anakumbukwa na raia wengi wa China, hata kama alikua mtua asiye shauriwa na mwenye kiburi na udikteta, ambaye kampeni zake za kisiasa ziliwaua mamilioni ya watu, katika miaka ya 1958-1962 katika muongo wa Mapinduzi ya kitamadunii, yaliyozinduliwa mwaka 1966.

Kiongozi wa sasa Xi Jingping ameikaribisha kazi nzuri aliyoifanya Mao Tse-tung katika utawala wake licha ya Chama cha Kikomunisti kutambua katika miaka ya 1980 "makosa yaliotendwa miaka iliyopita".

Kama watumiaji wengi wa mitandao mbalimbali wamekaribisha jitihada hizo, wengine wamekosoa sanamu hiyo, wakisema kuwa imejengwa katika mkoa ambapo janga la njaa, liliwaua mamilioni ya watu, katika miaka ya 50.