UKRAINE-URUSI

Ukraine yataka kurejesha kwenye himaya yake maeneo iliyopoteza

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko, Desemba 15, 2015, Kiev.
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko, Desemba 15, 2015, Kiev. GENYA SAVILOV / AFP

Ukraine inatarajia kurejesha kwenye himaya take kuanzia mwaka 2016 udhibiti wa maeneo yanayoshikiliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Ukraine pia inataka kuunda utaratibu wa kimataifa utakaozishirikisha Brussels na Washington ili kurejesha kwenye himaya yake eneo la Crimea lililounganishwa na Urusi, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema Alhamisi hii.

"Mwaka 2016, uhuru wa Uraine utarejeshwa katika maeneo ya mikoa ya Donetsk na Lugansk inayosikiliwa na waasi", ambapo vita vimesababisha zaidi ya watu 9,000 kupoteza maisha tangu Aprili mwaka 2014, Bw Poroshenko amesema, huku akiahidi kutumia tu uwezo wa kisiasa na kidiplomasia kwa kufanikisha hilo.

Kuhusu eneo la Crimea lililounganishwa kwa Urusi mwezi Machi 2014, Kiev ina mpango wa "kupendekeza kuanzisha utaratibu wa kimataifa ili kumaliza hali hiyo", Rais Poreshenko ameongeza.

Moscow na Kiev zinaendelea kukabiliwa na mgogoro mkubwa tangu kuingia madarakani nchini Ukraine kwa mtu anayeungwa mkono na nchi za magharibi mwanzoni mwa mwaka 2014, na kufuatiwa na kuunganishwa kwa eneo la Crimea kwa Urusi kufuatia kura ya maoni yenye utata, kisha mgogoro wa kuyatenga na Ukraine maeneo yanayoshikiliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi, mashariki mwa Ukraine.