IRAN-MAREKANI-VIKWAZO

Iran yalaani vikwazo vipya vya Marekani baada ya mkataba wa nyuklia

Katibu mkuu wa IAEA, Yukiya Amano (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif (kulia) na mkuu wa wa sera za nje wa Ulaya Federica Mogherini, Januari 17, 2016 mjini Vienna.
Katibu mkuu wa IAEA, Yukiya Amano (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif (kulia) na mkuu wa wa sera za nje wa Ulaya Federica Mogherini, Januari 17, 2016 mjini Vienna. AFP/APA/AFP

Jumatatu hii Iran imetangaza vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya mpango wake wa makombora, huku ikiendelea na mazungumzo yake juu ya utekelezaji wa makubaliano ya kihistoria kuhusu makubaliano ya nyuklia.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Yukiya Amano, amewasili mjini Tehran ambapo amepokelewa na Rais Hassan Rouhani Jumatatu hii mchana.

Jumamosi IAEA iliruhusu utekelezaji wa makubaliano yalioafikiwa mwezi Julai kati ya Iran na mataifa yenye nguvu, ikisisitiza kuwa Tehran imetekeleza ahadi zake kwa ajili ya kuondolewa vikwazo vya kimataifa.

Lakini shauku hiyo imevurugwa na vikwazo vipya vilivyotangazwa Jumapili na Marekani kwa kupinga mpango wa makombora wa Iran.

Vikwazo hivi ni vya kiwango kidogo kwa sababu vinawahusu raia wa watano kutoka Iran na mtandao wa makampuni yaliopo katika Umoja wa Falme za Kiarabu na China, ambayo yaliongezwa kwenye orodha ya kifedha ya Marekani iliyopigwa kalamu, kwa mujibu wa Hazina mjini Washington.

Tehran iliita vikwazo hivyo Jumatatu hii kuwa si "halali" kwa sababu "mpango wa makombora wa Iran haukuanzishwa kwa kuwa na uwezo wa kubeba nyuklia", Hussein Jaber Ansari, msemaji wa Wizara ya mambo ya Nje ya Iran amesema.