UKRAINE-URUSI-SHERIA

Kiev yaomba Moscow "kumuachia huru mara moja" Nadia Savchenko

Rubani wa Ukraine Nadia Savchenko, akiwa katika mgomo wa kususia chakula wakati wa kusikilizwa kwake katika mahakama ya Donetsk, Machi 9, 2015.
Rubani wa Ukraine Nadia Savchenko, akiwa katika mgomo wa kususia chakula wakati wa kusikilizwa kwake katika mahakama ya Donetsk, Machi 9, 2015. AFP

Jumatano wiki hii, Ukraine imetaka "aachiwe huru mara moja rubani wake" Nadia Savchenko, aliyehukumiwa nchini Urusi kwa kosa la mauaji ya waandishi wa habari wawili katika eneo la mashariki mwa Ukraine lililojitenga. Nadia Savchenko ameendelea na mgomo wake wa kususia chakula.

Matangazo ya kibiashara

"Tunauomba upande wa Urusi kuwaachia huru mara moja wafungwa wote wa kisiasa wa Ukraine, akiwemo Nadia Savchenko na kuachana na utaratibu huo wa kisheria ambao umepitwa na wakati ", ameandika kwenye Twitter msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine Mariana Betsa.

Ofisi ya mashitaka ya Urusi ilimuombea Nadia Savchenko adhabu ya kifungo cha miaka 23 gerezani, hukumu ambao inatazamiwa kutolewa Machi 21 na 22.

Nadia Savchenko, alichukua uamuzi huo wa kususia chakuala na vinywaji tangu wiki moja iliyopita.