JAPAN-NYUKLIA

Abe: "Japan haiwezi kutumia nishati ya atomiki"

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe katika mkutano na waandishi wa habari Tokyo, Machi 10, 2016.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe katika mkutano na waandishi wa habari Tokyo, Machi 10, 2016. AFP

Japan hawezi kutumia nishati ya nyuklia, amesema Alhamisi hii Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe katika mkutano na waandishi wa habari siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 5 ya maafa yaliosababidshwa na atomiki katika jimbo la Fukushima.

Matangazo ya kibiashara

"Nchi yetu maskini katika raslimali haiwezi kutumia nishati ya nyuklia kwa kuhakikisha ugavi wa kutosha wa nishati, kwa kuzingatia masuala ya kiuchumi na mabadiliko ya tabia nchi," amesema katika mjadala wa kufufua mitambo ya kuzalisha nishati ya nyuklia.

Baada ya hotuba ya dakika kumi na tano kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mkoa uliokumbwa na tsunami Machi 11, 2011, Bw Abe aliulizwa kuhusu sera ya nyuklia siku moja baada ya amri ya kusimamishwa kwa mitambo miwili ambayo imekua imeanza kufanya kazi.

"Mamlaka ya Udhibiti wa Nyuklia iliamua hivi karibuni kuwa mitambo hiyo inaendana na viwango vyake vya kiusalama ambavyo vinazingatiwa kwa umakini zaidi duniani, kwa kuzingatia vigezo vya kiufundi na kisayansi," amesisitiza Abe, akiongeza kuwa "hakuna mabadiliko" katika suala hilo.

Alisisitiza mara kadhaa kwamba sera ya serikali ilikuwa kuruhusu kuanzisha upya "mitambo yote ya nyuklia ambayo inaonekana salama na taasisi hii huru."

Hivi sasa, kunasalia mitambo 43 ya nyuklia inayoweza kufanya kazi nchini Japan (dhidi ya 54 kabla ya ajali Fukushima), lakini mitambo 2 pekee ndio inafanya kazi. Mitambo mingine 2 (Takahama 3 na 4) ilikua ilianza kufanya kazi, lakini vyomvo vya sheria viliamuru isimamishwe.

Abe pia ameahidi "dhamira kamili ya serikali juu ya suala la maji machafu katika kiwanda cha Fukushima" na kuruhusu mkoa kujidhatiti.

Raia wengi wa Japan wametoa hisia zao wakionekana kupinga kwa kuanzishwa kwa mitambo hiyo, kulingana na utafiti uliokua ukiendeshwa mara kwa mara na vyombo vya habari.

Japan, ambayo ni ya sitakwa kutoa gesi chafu, imeahidi kupunguza uzalishaji wake kwa 26% kati ya 2013 na mwaka 2030.

Ili kufikia lengo hili, nishati ya nyuklia inapaswa kutoa 20 hadi 22% ya umeme, kulingana na ahadi iliyotolewa na Tokyo kwa Umoja wa Mataifa. uwiano ilikuwa ulikua kutoka 25% hadi 30% kabla ya ajali.

Nishati mbadala itaongezwa kiwango kutoka 22% hadi 24% kwa mwaka wa fedha 2030 (Aprili 2030-Machi 2031), dhidi ya 11% kwa mwaka uliomalizika mwishoni mwa Machi 2014.