BURMA-SUU KYI-SIASA

Burma: Aung San Suu Kyi apendekezwa kuwa waziri

Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha LND Burma, Rangoon, le Novemba 9,2015.
Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha LND Burma, Rangoon, le Novemba 9,2015. REUTERS/Jorge Silva

Aung San Suu Kyi, ambaye hakuweza kuwa rais kwa sababu ya katiba iliyoandikwa na utawala wa kijeshi, anatazamiwa kujiunga katika serikali ya Burma, kwa mujibu wa tangazo lililotolewa bungeni Jumanne hii.

Matangazo ya kibiashara

"Hii hapa ni orodha ya wale ambao wanapaswa kuwa mawaziri, iliyowasilishwa bungeni na rais mpya aliyechaguliwa," Htin Kyaw, mshirika wa karibu wa Aung San Suu Kyi, amesema mbele ya Wabunge Spika wa Bunge, Mann Than Win Khaing.

Amekariri majina, ikiwa ni pamoja na lile la mpinzani, ambaye chama chama chake kina Wajumbe wengi Bungeni.

Hata hivyo hakueleza nafasi ambayo Aung San Suu Kyi atashikilia katika Baraza la Mawaziri, ambalo litaanza shughuli zake mwishoni mwa mwezi Machi na mapema mwezi Aprili.

Uvumi unaozagaa mitaani unasema kuwa kiongozi huyo mkuu wa upinzani huenda akashikilia nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje, nafasi ambayo itamruhusu kuiwakilisha nchi yake katika jukwaa la kimataifa.

Baraza hili la mawaziri litakaloundwa na raia wa kawaida ni la kwanza nchini Burma kwa miongo kadhaa.

Aung San Suu Kyi aliamua kumuweka Htin Hyaw, ambaye hajulikani katika nchi za kigeni, kwa nafasi ya Rais, ambayo katika ndoto zake alikua akifikiria kuishikilia.

Lakini Katiba inapiga marufuku nafasi hiyo kushikiliwa na mtu mwenye watoto wenye uraia wa kigeni, kesi inayomkuta Aung San Suu Kyi, ambaye ana watoto wawili wenye uraia wa Uingereza.