ICTY-YUGOSLAVIA-KARADZIC-SHERIA

Radovan Karadzic ahukumiwa kifungo cha miaka 40 jela na ICTY

Radovan Karadzic alikuwepo wakati wa uamuzi wa kesi yake kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Yugoslavia ya zamani Machi 24, 2016.
Radovan Karadzic alikuwepo wakati wa uamuzi wa kesi yake kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Yugoslavia ya zamani Machi 24, 2016. REUTERS/Robin van Lonkhuijsen

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Yugoslavia ya zamani (ICTY) imetbitisha Alhamisi hii Machi 24, 2016 kuwa aliyekuwa kiongozi wa kisiasa wa Waserbia wa Bosnia, Radovan Karadzic, amepatikana na hatia ya mauaji ya kimbari ya Srebrenica.

Matangazo ya kibiashara

Radovan karadzic pia anakabiliwa na hukumu zingine tisa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, na amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela.

Radovan Karadzic amesema atakata rufaa. Mtuhumiwa huyo yuko chini ya ulinzi tangu Julai 21, 2008. Chini ya Ibara ya 101C, kipindi chote hicho amesalia jela kitakatwa kutoka adhabu yake. Kwa mujibu wa Ibara 103C, mshitakiwa ataendelea kuzuiliwa na Mahakama kwa kusubiri kukamilika kwa maelezo kuhusu kuhamishwa kwake katika nchi nyingine ambapo atatumikia adhabu yake.

Hili ni hitimisho la kesi ndefu tangu miaka 7 iliyopita. Radovan Karadzic alikamatwa mwaka 2008 wakati alikuwa mafichoni katika mji wa Belgrade. Baada ya miaka kumi na moja akiwa mafichoni, alifikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Yugoslavia ya zamani mjini Hague.

Alhamisi hii Machi 24, Karadzic amekutwa na hatia ya mauaji ya kimbari kwa ya Srebrenica katika majira ya joto 1995 pamoja na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, hasa kwa kuzingirwa kwa mji wa Sarajevo na kutekwa nyara kwa askari na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika majira ya joto 1995, wakati ambapo jeshi la Waserbia la Bosnia lilipoanza kushindwa vita dhidi ya askari wengine wa kiislamu na jamii ya raia kutoka Croatia katika Ukanda huo.

Radovan Karadzic atatumikia kifungo cha miaka 40 jela, adhabu nzito ambayo haijawahi kuchukuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Mtuhumiwa Tayari ametangaza kwamba atakata rufaa kwa uamuzi huo. Kamishna mkuu ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ameutaja uamuzi huo wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Yugoslavia ya zamani kuwa ni wa "muhimu sana".