JAPAN-NYUKLIA-G7

Mawaziri kutoka G7 katika eneo la Makumbusho la Hiroshima

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za G7 katika eneo la Makumbusho ya Hiroshima Aprili 10, 2016.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za G7 katika eneo la Makumbusho ya Hiroshima Aprili 10, 2016. Reuters

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za G7, ikiwa ni pamoja na John Kerry, wametembelea Jumatatu hii katika makavazi ya Hiroshima, kwa kutoa heshima kwa wahanga wa bomu la atomiki la Marekani lililopigwa katika mji huo wa Japan mwaka 1945.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amewasili katika eneo hilo la makumbusho na kuanza ziara yake yenye ishara na isiyokuwa ya kawaida akiambatana na wenzake kutoka nchi zenye nguvu za G7, waandishi wa habari wamebainisha.

John Kerry ni kiongozi wa kwanza serikalini nchini Marekani kufika katika mji wa Hiroshima tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na mashambulizi ya kwanza ya atomiki katika historia ya nchi hizo mbili, Agosti 6, 1945.

Alipoulizwa Jumapili hii usiku ili kujua iwapo Bw Kerry ataelezea masikitiko yake, mwanadiplomasia mmoja wa Marekani alisema asingeweza kuwasilisha "msamaha" rasmi lakini waziri, kama "Wamarekani wote na Wajapani, wamejaa na huzuni" .

Akipokelewa Jumatatu hii asubuhi na mwenyeji wa mkutano wa nchi za G7, mwenzake wa Japan Fumio Kishida, John Kerry kwa mara nyingine tena ameonyesha matumaini kwamba "tutakuwa na uwezo ili kuondoa silaha za maangamizi uimwenguni."

Utawala wa Obama una nia njema tangu mwaka 2009 kwa kujikita na kazi ya kupokonya silaha na kazi nyingine muhimu, hadi kufikia "dunia isio kuwa na silaha za nyuklia."

Kerry anahudhuria tangu Jumapili mikutano ya Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za G7 (Marekani, Japan, Canada, Ufaransa, Uingereza, Italia, Ujerumani) inayofanyika mwaka huu katika mji wa Hiroshima, kwa mujibu wa matakwa ya Japan.