UFILIPINO-MATEKA

Wanamgambo wa Kiislam watishia kuwaua mateka 3 Ufilipino

Rais wa Ufilipino, Benigno Aquino katika kambi ya jeshi la anga, Angeles city, Pampanga DIsemba 21,2015.
Rais wa Ufilipino, Benigno Aquino katika kambi ya jeshi la anga, Angeles city, Pampanga DIsemba 21,2015. Reuters

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Abu Sayyaf limerusha hewani Jumanne hii video inayowaonyesha mateka watatu, kutoka Canada, Norway na Ufilipino, na kutishia kuwaua, wiki mmoja baada ya kumua raia moja wa Canada aliyetekwa nyara pamoja nao.

Matangazo ya kibiashara

Katika video hiyo, iliyorushwa Jumanne hii kwenye YouTube,mateka hao watatu tatu, kutoka Canada Robert Hall, Norway Kjartan Sekkingstad, na Ufilipino Marites Flor, rafiki wa Bw Hall, wametoa wito kwa serikali za Canada na Ufilipino, wakiomba "kutekeleza madai ya kundi hilo", shirika maalum katika ufuatiliaji wa vyombo vya habari vya jihadi SITE, limearifu.

Mateka hao wameonekana wakikaa chini, nyuma ya shamba la linaloonekana kuwa la nazi, chini ya ulinzi wa watu sita wenye silaha wakisimama nyuma yao.

Mateka kutoka Canada, Robert Hall, anasema watekaji nyara wamemuamuru kuomba serikali ya Canada na "kutekeleza" mahitaji yao, bila kuyabainisha.

Mateka kutoka Norway, Kjartan Sekkingstad, amesisitiza kwamba kama "madai hayo hayatotekelezwa, tutauawa siku chache kama rafiki yetu John."

Mmoja wa watekaji nyara ameonya serikali ya Ufilipino naupata "somo" katika mauaji ya John Ridsdel na kuepukakuchelewa katika mazungumzo hayo.

Kundi hili wanamgambo wa Kiislamu la Abu Sayyaf lilitangaza wiki iliyopita kuwa lilimuua mateka kutoka Canada John Ridsdel, baada ya kumalizika kwa muda uliyotolewa Aprili 25, kwa kutoa fidia ili aweze kuachiliwa huru.

Mateka hawa watatu walitekwa nyara mwishoni mwa mwezi Septemba pamoja na John Ridsdel, walipokuwa katika mgahawa kusini mwa Ufilipino.

Rais Ufilipino Benigno Aquino aliahidi mwishoni mwa mwezi Aprili kuanzisha mashambulizi ya kijeshi kwa lengo la "kutokomeza shughuli za kihalifu" za kundi la Abu Sayyaf na kuonya kuwa serikali haitojadiliana na shirika inalolichukulia kama la kigaidi.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau pia ametupilia mbali mazungumzo yoyote na watekaji nyara.

Bw Aquino alisema kuwa mateka wanashikiliwa katika kisiwa cha Jolo, ngome kuu ya jadiya kundi la Abu Sayyaf, zaidi ya kilomita elfu kusini mwa Manila.