KOREA KASKAZINI-KONGAMANO

Korea ya Kaskazini: kongamano la kwanza la chama tawala

Korea ya Kaskazini Ijumaa hii inaanzisha mkutano wake mkubwa wa kwanza wa kisiasa baada ya miaka karibu 40, mkutano wa chama kimoja pekee madarakani.

Kongamano la kwanza baada ya miaka 40 Korea Kaskazini.
Kongamano la kwanza baada ya miaka 40 Korea Kaskazini. AFP
Matangazo ya kibiashara

Madhumuni ya mkutano huo ni kuhakikisha utawala wa kudumu wa Kim Jong-Un, pamoja na kuongezeka kwa uwezekano wa majaribio mengine ya nyuklia.

Maelfu ya wajumbe kutoka maeneo mbalimbali ya Korea ya Kaskazini wamejielekeza mjini Pyongyang kuhudhuria mkutano huu wa kipekee wa Chama Wafanyakazi wa Korea (PTC).

Kim Jong-Un, mwenye umri wa miaka 33, alizaliwa baada ya tukio kama hilo, mwaka1980. Anatarajiwa kutoa hotuba ambayo itachunguzwa kwa karibu na waangalizi kwa kutafuta dalili zote za mabadiliko ya sera au watu miongoni mwa vigogo katika chama tawala.

Mwaka 1980, kongamano lilimteua baba yake Kim Jong-Il kama mrithi wa Kim Il-Sung, mwanzilishi wa udikteta wa kiukoo unaodumu karibu miaka 70.

Ajenda ya mkutano haijajulikana, wala muda wake. Lakini lengo kuu ni uwezekano wa kuimarisha utawala wa Kim Jong-Un kama kiongozi mkuu wa Korea ya Kaskazini na mrithi halali wa mababu zake na baba yake.

Kongamano hili pia litathibitisha kama sera ya chama, mkakati wa "byungjin" ulioanzishwa na Kim Jong-Un, yaani kuendesha sanjari maendeleo ya kiuchumi na mipango ya nyuklia pamoja na kombora ya masafa marefu.

- Sikukuu ya propaganda -

Wakati ukikaribiamkutano huo, bendera za chama tawala cha PTC na bendera ya taifa, zimewekwa mitaa mbalimbali ya mji wa Pyongyang. "Wandugu zetu wakubwa Kim Il-Sung na Kim Jong-Il watakuwa nasi daima," unaweza kusoma kwenye kusomayalitowekwa katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu.

Kiongozi kijana wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un alichukua hatamu ya uongozi wa nchi hiyo mwezi Desemba 2011 baada ya kifo cha baba yake. Korea Kaskazini tangu wakati huo hadi sasa imefanya makjaribioimawili ya nyuklia na majaribio mawili ya kurusha chombo hewani yaliyofaulu, ambayo talichukuliwa kama majaribio yaliyojificha ya kombora ya masafa marefu.