Maelewano ya kidiplomasia baada ya vurugu Karabakh
Imechapishwa:
Urusi na Marekani, Jumatatu hii Mei 16, waliwashinikiza marais wa Armenia na Azerbaijan kuimarisha mkataba tete wa usitishwaji wa mapigano katika eneo la mgogoro la Nagorno-Karabakh, ambapo hali ya usalama ilizorota mwezi uliopita kutokana na mapigano makali.
Marais wa Armenia, Serzh Sargsyan na Azerbaijan Ilham Aliyev walikutana mapema jioni katika hoteli ya mjini Vienna akiwepo Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, na Waziri wa Mambo ya Ulaya wa Ufaransa, Harlem Desir.
Marais hao wawili hawajakutana tangu kuanza kwa mzozo katika eneo la Karabakh, takriban robo karne. Eneo hili lilikumbwa na ongezeko la machafuko yaliyogharimu maisha ya watu wasiopungua 110 mwezi Aprili. Raia wa kawaida na wanajeshi kutoka nchi hizi mbili ni miongoni mwa watu waliouawa katika machafuko hayo. Armenia na Azerbaijan ni moja ya sehemu za nchi zilizokua zikiunda Urusi ya zamani kusini mwa Caucasus.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alikutana na kila mmoja wa marais hawa.
Mwanadiplomasia mwandamizi wa Marekani, Jumatatu hii, ameonyesha matumaini yake, akisema ni "mgogoro ambao unaweza kupatiwa ufumbuzi" na ambapoo matokeo yanaweza kuwa "mazuri kwa pande zote mbili."
Mapigano ya mwezi Aprili yalikua mapigano mabaya tangu makubaliano ya kwanza ya kusitisha mapigano mwaka 1994 baada ya vita vilivyogharimu maisha ya watu 30,000 na kusababisha mamia ya maelfu ya wakimbizi, wengi wao wakiwa raia wa Azerbaijani.
Moscow na matumaini kwamba mkutano huu si tu kusaidia na "utulivu" Hali lakini pia kuanzisha upya mazungumzo juu ya hadhi ya Nagorno-Karabakh, mkoa wakazi na idadi kubwa ya Waarmenia ilijitoa lakini hiyo bado inatambulika kimataifa kama kufanya sehemu ya Azerbaijan.