KOREA-KUSINI-BAN

Ban Ki-moon kuitembelea nchi yake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alifanya ziara yake ya tatu ya kikazi nchini Burkina Faso, Mwanzoni mwa Machi 2016.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alifanya ziara yake ya tatu ya kikazi nchini Burkina Faso, Mwanzoni mwa Machi 2016. © REUTERS/Denis Balibouse

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anatarajiwa kuanza ziara ya siku sita katika nchi yake ya Korea Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema ziara hii pia inalenga kuweka mikakati ya Moon kuwania urais nchini humo katika siku zijazo baada ya kustaafu kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Moon mwenye umri wa miaka 71 anatarajiwa kustaafu kufikia mwisho wa mwaka huu, miezi 12 kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao nchini ya nchi yake.

Amekuwa akipata uugwaji mkono nchini mwake kutokana na wadhifa alio nao wa Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.