Nadiya Savchenko, rubani wa Ukraine aachiliwa huru
Imechapishwa:
Rubani wa Ukraine, Nadiya Savchenko, aliyekua akizuiliwa nchini Urusi ameachiliwa huru katika zoezi la kubadilishana wafungwa baada ya Ukraine pia kuwaachilia huru askari wawili wa Urusi waliokua wakizuiliwa nchini Ukraine.
Baada ya tu ya kuachiliwa huru, Savchenko amesema yuko "tayari kujitolea kwa mara nyingine kwa ajili ya Ukraine." Rais Poroshenko alikwenda mwenyewe katika mji wa Rostov-sur-le-Don kumtafuta rubani huyo mwanamke ambaye amechukuliwa kama shujaa nchini Ukraine. Nadiya Savchenko alihukumiwa mwezi Machi nchini Urusi kifungo cha miaka 22 jela.
Nadiya Savchenko amepokelewa katika mji wa Kiev kwa vifijo na deremo na umati wa watu pamoja na waandishi wa habari wa Ukraine ambao wamekua wakishrehekea shujaa wao wakati ambapo askari wawili wa Urusi wamekua wakiwasili mjini Moscow.
Vyombo vya habari vya Urusi, ndio vilikua vya kwanza kutaja kuwasili kwa ndege iliyokuwa imewabeba askari wawili wa Urusi ambao hivi karibuni walihukumiwa na vyombo vya sheria vya Ukraine kwa kushiriki katika operesheni ya siri mashariki mwa Ukraine, mwandishi wetu katika mji wa Moscow, Muriel Pomponio, amearifu. Taarifa hii imethibitishwa na mwanasheria wao kutoka Ukraine: "Evgueni Eerofeiev na Alexander Alexandre hawapo tena nchini Ukraine," amesema.
Katikati ya mchana ndege ya Rais wa Ukraini ilimsafirisha Nadiya Savchenko kutoka Moscow hadi uwanja wa ndege wa Boryspil karibu na mji wa Kiev, kwa mara ya kwanza tangu miaka miwili iliyopita, mwandishi wetu katika mji wa Kiev, Stéphane Siohan, ameelezea.