Obama aandaa ziara yake ya kihistoria Hiroshima
Imechapishwa:
Ziara ya Barack Obama katika mji wa Hiroshima Ijumaa hii, ni ziara ya kwanza ya rais wa Marekani aliye madarakani katika mji huo uliokumbwa, mwaka 1945, na mashambulizi ya mabomu mawili ya nyuklia ya Marekani.
Akizungumzia ziara yake ya Hiroshima, ambapo watu 140,000 waliuawa asubuhi ya Agosti 6, 1945, Bw Obama alizungumzia katika mkutano na vyombo vya habari "hatari halisi iliyopo na hoja ya dharura ambayo watu wote wanapaswa kuwa nayo".
Silaha za nyuklia hazipewi kipau mbele kama wakati wa vita baridi lakini uwezekano wa "tukio la kinyuklia bado kumbukumbu zetu," Rais Barack Obama ameongeza.
Kwa hali hii, Korea ya Kaskazini, ambayo iliendesa Januari 6 jaribio lake la nne la nyuklia licha ya maazimio ya Umoja wa Mataifa ambayo yaliikataza, "ni chanzo kiliyo wazi ya wasiwasi wetu sote," amesema rais wa Marekani.
Mkutano wa Wakuu wa nchi au serikali kutoka Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Ujerumani, Canada na Japan unajikita katika ukuaji dhaifu wa kimataifa.