MALAYSIA-USAFIRI

Watu kadhaa wajeruhiwa katika ndege ya Malaysia Airlines

Abiria wakipiga foleni kwa kusubiri usafiri wa ndege ya Malaysia Airlines katika uwanja wa ndege wa kimtaifa wa mjini Kuala Lumpur Machi 9, 2014.
Abiria wakipiga foleni kwa kusubiri usafiri wa ndege ya Malaysia Airlines katika uwanja wa ndege wa kimtaifa wa mjini Kuala Lumpur Machi 9, 2014. Reuters/路透社

Abiria na wafanyakazi wa ndege yenye chapa A380 ya shirika la ndege la Malaysia Airlines wamepata majeraha madogo baada ya ndege hiyo waliyokuwemo kupatwa na mtikisiko mkubwa.

Matangazo ya kibiashara

Ndege ya Malaysia Airlines ilikua ikifanya safari Jumapili hii kati ya London na Kuala Lumpur, shirika la ndege la Malaysia Airlines limetangaza .

Ngege hii iliyokua na watu 378 kwenye ilipata na mtikisiko mkubwa kwa muda mfupi juu ya anga ya ghuba ya Bengale, katika bahari ya Hindi.

"Kutokana na mtikisiko mkubwa, abiria wamepata majeraha madogo. Idadi ndogo ya abiria na wafanyakazi wamehudumiwa kimatibabu na timu ya matabibu" walipowasili katika uwanja wa ndege wa mjini Kuala Lumpur, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la ndege la Malaysia Airlines.

Picha zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha jinsi mabaki ya chakula vinywaji na vifaa vingine vilivyokua vikidondoka kutoka katika sehemu ya mizigo.