UTURUKI-RSF

RSF yalaani kukamatwa kwa mwakilishi wake Uturuki

Erol Önderoglu wakati wa mkutano na waandishi wa habari Machi 2, 2016.
Erol Önderoglu wakati wa mkutano na waandishi wa habari Machi 2, 2016. OZAN KOSE / AFP

Nchini Uturuki, Jumatatu 20 Juni, Erol Onderoglu, mwakilishi wa shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka (RSF) nchi humo alishtakiwa kwa "propaganda ya kigaidi." Onderoglu ameshitakiwa na watu wawili mashuhuri, mwandishi Ahmet Nesin na Profesa wa Tiba Sebnem Korur Fincanci.

Matangazo ya kibiashara

Watatu hao wanashtumiwa kushiriki katika kampeni ya mshikamano pamoja na gazeti linalounga mkono Wakurdi la Ozgur Gündem.

Vyombo vya habari nchini Uturuki vinaendelea kukabiliwa na hali tete baada ya mwakilishi wa RSF kukamatwa Jumatatu kwa tuhuma za "propaganda ya kigaidi" pamoja na watu wawili mashuhuri wanaotuhumiwa kuwasaidia Wakurdi.

Wote watatu wamewekwa rumande kwa muda na kuna hatari wasaliye jela kwa miaka kadhaa.

Mahakama inamtuhumu Erol Onderoglu, anayewakilisha RSF tangu mwaka 1996 nchini Uturuki, pamoja na Ahmet Nesin na Bi Sebnem Korur Fincanci, kushiriki katika kampeni ya mshikamano na waandishi wa habari wanaounga mkono Wakurdi mwezi Mei.

Shirika la Waandishi wa Habari Wasiokuwa na Mipaka limeomba kuachiliwa huru kwa watu hao watatu. "Kwa upande wetu, ni wazi kwamba kukamatwa kwa Erol Onderoglu ni vitisho dhidi ya taaluma nzima, Johann Bihr, mkuu wa ofisi ya RSF katika Ulaya ya Kati na Asia, ameiambia RFI. Inabidi kujua kwamba Onderoglu ni mwakilishi wetu kwa miaka ishirini. Ni mtu ambaye ni mashuhuri duniani kote kwa ajili msimamo wake, mtazamo wake. Anafanya kazi mara kwa mara na mashirika ya kimataifa kama vile OSCE [Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya], hasa kwa kukusanya orodha ya waandishi wa habari wanaozuiliwa jela. Pia wanakusanya, ripoti kuhusu hali ya uhuru wa kujieleza kwenye tovuti ya habari ya Bianet, inayojikita juu ya haki za binadamu. Hivyo ni basi ,ni mtu mkubwa katika ulinzi wa uhuru wa vyombo vya habari ambaye amekamatwa. "

Shirika hilo linakumbusha kwamba Uturuki inachukua nafasi ya 151 kwa jumla ya nchi 180 katika katika uhuru wa vyombo vya habari