BURMA-JAMII

UN yatiwa wasiwasi na hali ya Waislamu wa Rohingya

Wanawake na watoto kutoka jamii ya Rohingya wakirudi kutoka hospitali ilio karibu na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kutupalong, katika wilaya ya Cox's Bazar, kusini mashariki mwa Burma.
Wanawake na watoto kutoka jamii ya Rohingya wakirudi kutoka hospitali ilio karibu na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kutupalong, katika wilaya ya Cox's Bazar, kusini mashariki mwa Burma. REUTERS/Rafiqur Rahman

Ukiukwaji wa haki za Waislamu wachache kutoka jamii ya Rohingya nchini Burma unaweza kuchukuliwa kama "uhalifu dhidi ya ubinadamu", kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyotolewa Jumatatu 20 Juni.

Matangazo ya kibiashara

Rohingya ni jamii ya watu wachache ya watu zaidi ya milioni moja, ikiwa ni pamoja na watu zaidi ya 100,000 wakiwa wamejazana katika makambi ya wakimbizi wa ndani tangu machafuko ya kijamii kutokea mwaka 2012. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kundi hili dogo linakabiliwa ikiwa ni pamoja na kunyimwa uraia, kazi za kulazimishwa na ukatili wa kijinsia.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ilitoa ripotiJumatatu hii Juni 20 kuhusu visa vya ukatili kwa watu walio wachache kikabila na kidini nchini Burma. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imekemea "mfululizo wa ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya watu kutoka jamii ya Rohingya [...] na kupendekeza kiasi kikubwa cha mashambulizi au utaratibu [...] ambao unaweza kusababisha mashtaka ya uwezekano wa uhalifu dhidi ya ubinadamu mbele ya mahakama" .

Rohingyas ni jamii ya watu wachache ya watu zaidi ya milioni moja wanaoishi nchini Burma. Hii ni moja ya jamii ya watu wachache zaidi kuteswa duniani. Baadhi yao wanaishi katika nchi hii kwa zaidi ya miaka 100, lakini bado wanachukuliwa kama wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya Bangladesh.

Katika jimbo la Arakan, liliyoko magharibi mwa Burma, zaidi ya watu 100,000 kutoka jamii ya Rohingyas bado wanaishi katika makambi ya wakimbizi wa ndani. Mwaka 2012, machafuko ya kijamii kati ya Mabudha na Waislamu yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 200, hasa Waislamu.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inabainisha kuwa watu kutoka jamii ya Rohingya wasiokuwa na uraia, wametengwa katika soko la ajira, katika mfumo wa elimu na afya na wanakabiliwa na vitisho kwa maisha yao na usalama, kazi ya kulazimishwa, na ukatili wa kijinsia. watoto kutoka jamii hii ya Rohingya hawapati cheti cha kuzaliwa tangu miaka ya 1990.