KOREA KASKAZINI-USALAMA

Korea ya Kaskazini yarusha makombora mawili ya masafa ya kati

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. KCNA/via REUTERS

Korea ya Kaskazini imerusha angani makombora mawili mfululizo ya masafa ya kati, kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Korea ya Kaskazini, ambayo imeeleza kwamba moja ya majaribio hayo imefeli, lakini kombora jingine limefaulu kwenda kwenye umbali wa kilomita 400.

Matangazo ya kibiashara

Vifaa vilivyorushwa vinasadikiwa kuwa makombora ya aina ya Musudan ya masafa ya kati ambayo yanaweza kutishia makambi ya jeshi la Marekani yaliopo katika kisiwa cha Guam, katika bahari ya Pasifiki.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imelaani vikali majaribio hayo, ikisema kwamba ni ukiukwaji wa wazi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa yanayoizuia Pyongyang kutumia teknolojia yoyote ya makombora.

Msemaji wa Waziri wa Umoja wa taifa wa Korea Kusini Joeng Joon-hee amesema majaribio hayo ni kukiuka vikwazo.

"Ulipuaji huo makombora kwa kutumia Teknolojia ya angani unakiuka maazimio ya Umoja wa mataifa. NIa ni uchokozi dhidi yetu. Tunashauri ni vyema kwa Korea Kaskazini kuzidisha nguvu katika kuimarisha amani katika eneo la rasi ya Korea na kwa maisha ya watu wake ambayo Korea kaskazini imekuwa ikisititiza kila wakati, " Joon-hee amesema.

Naye waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amelaani hatua hiyo Korea ya Kaskazini.
"Leo kumelipuliwa makombora kwa kutumia teknolojia ya angani iliyotumika zamani huu ni ukiukwaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa. hatutarusu na tutaandaa azimio la kupinga hatua hiyo," amesema Waziri Mkuu huyo

Jaribio la kwanza lilifanyika kabla ya saa 12 asubuhi saa za Korea ya Kaskazini ( sawa na saa 3 usiku saa za kimataifa) na kuna uwezekano kwamba lilishindwa. Lakini kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi, kombora la pili, lililorushwa saa mbili baadaye katika eneo hilo katika pwani ya mashariki lilikwenda umbali wa kilomita 400 juu Bahari ya Mashariki, pia inayojulikana kama Bahari ya Japan.