INDONESIA-SIASA

Indonesia: Hali ya sintofahamu Yogyakarta

AFP/GOH CHAI HIN

Hali ya sintofahamu imeibuka katika jimbo la Yogyakarta nchini Idonesia, baada ya mfalme wa jimbo hilo kutaka mwane wa kike amrithi kwenye uongozi wa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Hamengku Buwono X, Mfalme wa mwisho wa Indonesia ambaye pia ana uwezo wa kisiasa, amekua akikabiliana na baadhi ya wafuasi wake waliojitenga wakati wa sherehe za hivi karibuni za maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambaye ametimiza sasa miaka 70, pamoja na maadhimisho ya miaka 27 tangu ashikiliye enzi ya ufalme. Wengi miongoni mwa familia yake walisusia tukio hilo muhimu nchini Indonesia.

Mvutano huo ulianza kuibuka tangu Mfalme huyo asema mwishoni mwa mwaka 2015, kuwa anapanga kumteua binti yake mkubwa kumrithi. Mfalme huyo ana mabinti watano, na hakufanikiwa kumpata mtoto wa kiume.

Utawala wa kifalme wa Yogyakarta, ulioanzishwa mwaka 1756 katika mkoa wa kati wa Java una hadhi maalum tangu mwisho wa enzi za ukoloni katika miaka ya 1945. Itafahamika kwamba nchi ya Indonesia ilitawaliwa na Uholanzi.

Indonesia ni nchi yenye waislamu wengi, na ni marufuku mwanamke kushikilia uongozi wowote, wa kidini au wa kisiasa katika nchi hiyo.