Bangladeshi

Mateka 13 waokolewa kwenye mgahawa wa Dhaka

Walinzi wa mpaka karibu na mgahawa wa Dhaka ulioshambuliwa 1 Julai  2016.
Walinzi wa mpaka karibu na mgahawa wa Dhaka ulioshambuliwa 1 Julai 2016. Courtesy of Dhaka Tribune/Mahmud Hossain Opu

Mateka 13 wameokolewa kutoka katika mgahawa wa Dhaka ambapo wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislam walikuwa wamewakamata mateka baada ya Makomando wa Bangladeshi waliojihami vyema kwa sialaha kuvamia eneo hilo leo Jumamosi

Matangazo ya kibiashara

Mateka hao ikiwa ni pamoja na wageni watatu , kumi raia wa Bangladeshi, wameokolewa baada ya makabiliano makali ya risasi kati yao na polisi, maafisa wamesema.

Mpiga picha wa AFP ambaye yupo katika eneo la tukio amesema aliweza kusikia milio mikubwa ya risasi wakati vikosi vya usalama vilipozindua operesheni ya uokozi zaidi ya saa 10 baada ya wanamgambo hao kuwakamata mateka.

Mateka watano wameokolewa katika dakika chache za kuanza kwaoperesheni hiyo, amesema Tuhin Mohammad Masoud kamanda wa juu wa kikosi cha haraka cha makomando wasomi wa Bangladeshi ambao walivamia mgahawa huo.