Bangladeshi

Bangladeshi yakanusha kuwa na uhusiano na mitandao ya kimataifa ya wanajihadi

Askari wa Bangladeshi wakishika doria wakati wa operesheni ya polisi ili kuokoa  mateka katika mgahawa wa Dhaka, Julai 2 2016.
Askari wa Bangladeshi wakishika doria wakati wa operesheni ya polisi ili kuokoa mateka katika mgahawa wa Dhaka, Julai 2 2016. STR / APF / AFP

Serikali ya Bangladesh imesema kuwa washambuliaji waliowachinja mateka 20 katika mgahawa wa Dhaka walikuwa wafuasi wenye elimu wa kundi la wanamgambo wa ndani ambao wanaona itikadi za msimamo mkali kama "mtindo"wa kuigwa na kukanusha kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Wakati nchi hiyo ikianza siku mbili za maombolezo kwa ajili ya waathirika, taarifa za kina zimepatikana kuhusu jinsi washambuliaji hao walinusuru maisha ya Waislamu wakati wakitekeleza vifo vya wageni.

Waziri Mkuu Sheikh Hasina ameapa kuiondoa Bangladesh katika hali hiyo mbaya na kuonya kuhusu jitihada za pamoja zenye lengo la kuliangusha taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu duniani, wakati serikali yake ikiendelea kukanusha uhusiano kati ya shambulio hilo na mitandao ya kimataifa ya wanajihadi.

Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulizi hilo, na kusema kuwa lililenga mikusanyiko ya wananchi katika mikusanyiko ya kisiasa katika mgahawa wa kigeni usiku wa Ijumaa.