UGAIDI-IRAQ

Watu zaidi ya 70 wauawa katika shambulizi la kigaidi nchini Iraq

Mashambulizi ya kigaidi mjini Baghdad
Mashambulizi ya kigaidi mjini Baghdad REUTERS/Khalid al Mousily

Watu zaidi ya 70 wameuawa na wengine zaidi ya 130 wamejeruhiwa baada ya kundi la Islamic State kutekeleza shambulizi la kigaidi mjini Baghdad nchini Iraq.

Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini humo wanasema lililokuwa na mabomu lilipuka karibu na mkahawa uliokuwa na idadi kubwa ya wateja huku wengine wakiwa wapita njia katika Wilaya ya Karrada.

Wakati shambulizi hilo likitokea, mamia ya watu walikuwa wanafanya manunuzi kuelekea kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo.

Ripoti zinasema kuwa shambulizi lingine la pili lilitokea Kaskazini mwa jiji la Baghdad na kuwalenga Waislamu wenye mrengo wa Kishia.

Shambulizi la leo ni baadhi ya mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini Iraq mwaka huu.

Mauaji haya yamekuja wiki moja baada ya wanajeshi wa serikali kuuteka mji wa Falluja kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State.

Kundi hilo la Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi hilo huku ripoti zikisema kuwa idadi kubwa ya watoto wameauawa baada ya shambulizi hilo.