KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Pyongyang kuvunja mawasiliano na Washington

Picha iliyorushwa na shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini (KCNA) na inaonyesha kombora la masafa marefu lililorushwa Februari 7, 2016 na Korea Kaskazini.
Picha iliyorushwa na shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini (KCNA) na inaonyesha kombora la masafa marefu lililorushwa Februari 7, 2016 na Korea Kaskazini. REUTERS/KCNA

Korea ya Kaskazini imetangaza kwamba itasitisha mawasiliano na Washington. Nchi hiyo inapinga dhidi ya vikwazo vya Marekani vinavyomlenga kiongozi wake Kim Jong-un.

Matangazo ya kibiashara

Ni kutoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini ameionya serikali ya Marekani: "Tumewataarifu tutasitisha moja kwa moja mawasiliano rasmi ".

Hivi karibuni Marekani ilimuorodhesha Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, katika orodha ya wale waliopigwa marufuku kutokana na rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu.

Korea imesema kuwa maswala ambayo bado yanajadiliwa ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa raia wawili wa Marekani yatajadiliwa chini ya sheria kali za kivita.

Marekani na Korea Kusini zimetangaza mipango ya kuweka Mfumo wa ulinzi wa “Terminal High Altitude Area Defense (THAAD)” unaolenga kudungua makombora ya masafa marefu ya Korea kaskazini.

Korea kaskazini imbaini kwamba hatua hiyo iko wazi kwa nchi hizo mbili kuichokoza na hivyo kuamua kutangaza vita dhidi yao.

Hata hivyo Korea Kaskazini imeapa kudungua manuari yeyote ya kivita itakayolenga roketi zake za masafa marefu.