UN-UKRAINE

UN yataka waliohusika na machafuko Ukraine wakamatwe

Umoja wa Mataifa unasema, hakuna aliyechukuliwa hatua kutokana na machafuko yaliyotokea Mashariki mwa Ukraine mwaka 2014 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 9, baada ya vikosi vya Urusi kuvamia eneo hilo.

Shada za maua zikiwekwa kwenye mabaki ya MH17, ndege ya Malaysia Airlines, Julai 26, 2014, Grabove katika jimbo la Donetsk, Ukraine.
Shada za maua zikiwekwa kwenye mabaki ya MH17, ndege ya Malaysia Airlines, Julai 26, 2014, Grabove katika jimbo la Donetsk, Ukraine. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema matukio mengine yaliyotokea Mashariki mwa Ukraine, yalikuwa ni uhalifu wa kivita lakini hakuna aliyechukuliwa hatua.

Ripoti ya Tume hiyo inasema pia kuwa hata baada ya kumalizika kwa mauaji hayo, zaidi ya watu 47 wameuawa na wengine wametoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Tangu mwaka 2014, majimbo ya Donetsk na Luhansk, yanaendelea kushikiliwa na vikosi vya Urusi baada ya raia wa eneo hilo kusema wanataka kutaliwa na Moscow.