AUSTRALIA- USALAMA

Mtu mmoja akamatwa Australia akijaribu kufanya shambulizi

Polisi ya Australia imetangaza Alhamisi hii kwamba imemkamata mtu ambaye anadaiwa kujaribu kufanya shambulizi dhidi ya kituo cha polisi cha mjini Sydney alipokua akiingia kwenye kituo cha magari chini ya akitendesha gari lililokua limebeba mitungi ya gesi, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo.

Polisi ya Autralia ikiendesha msako ndani ya gari iliyokua ikibeba mitungi ya gesi, Sydney, Julai 21, 2016.
Polisi ya Autralia ikiendesha msako ndani ya gari iliyokua ikibeba mitungi ya gesi, Sydney, Julai 21, 2016. REUTERS/AAP/Sam Mooy
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukamatwa, polisi imetenga Alhamisi hii eneo la usalama kando ya kituo cha polisi kinachopatikana katika kata ya Merrylands, magharibi mwa jimwa Sydney, wakati ambapo kikosi cha polisi cha kutegua mabomu kitengo kilikua kikiendesha msako katika gari hilo.

Hakuna askari polisi au raia alijeruhiwa, polisi ya mji wa New South Wales imesema.

Mtu mmoja alikuwa namitungi ya gesi katika gari lake na amejichoma moto moto kabla ya kukamatwa, vyombo vya habari vimearifu, vikinukuu vyanzo vya polisi.

Australia, mshirika wa Marekani, iko katika hali ya tahadhari ili kuchunguza matukio ya msimamo mkali katika ardhi yake tangu mwaka 2014. Mashambulizi kadhaa tayari yalitokea nchini humo, hasa katika mgahawa mmoja mjini Sydney, ambapo mateka wawili waliuawa.