JAPAN

Walemavu 19 wauawa nchini Japan kwa kudungwa kisu

Kituo cha walemavu kilichovamiwa
Kituo cha walemavu kilichovamiwa 路透社

Watu 19 wameuawa baada ya kudungwa kisu katika kituo maalum cha kuwapa hifadhi walemavu katika mji wa Sagamihara nchini Japan.

Matangazo ya kibiashara

Matukio kama haya sio kawaida nchini humo, na ni tukio ambalo limeshangaza wengi kwa kuwa mauaji mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo kwa muda mrefu.

Polisi wanamshikilia mtu mmoja baada ya kwenda katika kituo cha polisi na kukiri kuwa alitekeleza shambulizi hilo.

Mwanaume huyo ambaye aliwahi kuwa mfanyikazi katika kituo hicho amesema, alitekeleza kitendo hicho kwa sababu alitaka watu wenye ulemavu watoweke kabisa.

Serikali ya Japan imesema imesikitishwa mno na mauaji haya, huku Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Yoshihide Suga akisema watu wasiokuwa na hatia wamepoteza maisha.

Polisi wanasema mwezi Februari mwaka huu, mtu huyo aliwaandikia barua wanasiasa nchini humo akitishia kuwauwa watu wenye ulemavu.

Baada ya barua hiyo alikamatwa na kupelekwa hospitali kupata matibabu ya akili lakini baada ya wiki mbili akaachiliwa huru.