UTURUKI-ERDOGAN

Uturuki: majenerali 149 wafutwa kazi

Rais wa Uturuki Erdogan ataongoza kikao cha baraza la kijeshi Alhamisi hii Julai 28, 2016.
Rais wa Uturuki Erdogan ataongoza kikao cha baraza la kijeshi Alhamisi hii Julai 28, 2016. REUTERS/Umit Bektas/File Photo

Nchini Uturuki, vyombo vya habari kwa mara nyingine tena na hali ya sintofahamu Jumatano hii , Julai 27 katika operesheni kabambe iliyoanzishwa na serikali baada ya mapinduzi kushindwa.

Matangazo ya kibiashara

Katika operesheni hiyo majenerali kadhaa wamefutwa kazi ikiwa ni pamoja na maafisa wa juu katika jeshi la majini. Pia baadhi ya magazeti yamefungwa.

Siku kumi na tatu baada ya kushindwa kwa mapinduzi nchini Uturuki, operesheni ya ya kamata kamata inaendelea katika taasisi mbalimbali za nchi na dhidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanadaiwa kuwa na ukaribu na imam Fethullah Gulen, anayetuhumiwa na serikali ya Uturuki kuratibu mapinduzi hayo yaliyoshindwa.

Waziri Mkuu ametangaza Jumatano wiki hii kwamba operesheni ya kamata kamata haijamalizika. Matangazo yalichapishwa katika gazeti la serikali. Serikali ya imeamuru kufungwa kwa vyombo vya habari kadhaa ikiwa ni pamoja na magazeti, runinga, redio, na mashirika matatu ya habari. Vyombo hivi vya habari vina ukaribu na imam Fethullah Gulen, ingawa baadhi ya vichwa vya habari vinaonekana kuwa na upinzani dhidi ya Rais Erdogan.

serikali ya Kituruki pia imefanya operesheni kabambe katika jeshi ambapo majenerali 149, sawa na nusu ya majenerali wa jeshi la Uturuki wamefutwa kazi. Itafahamika kwamba maafisa zaidi ya 700 na mamia ya maafisa wa ngazi za chini walifukuzwa kazi.

Baraza la kijeshi litakutana Alhamisi hii asubuhi chini ya uenyekiti wa Recep Tayyip Erdogan kwa lengo la kupanga upya uongozi wa majeshi ya Uturuki.