UTURUKI-IS

Uturuki yapoteza askari wake watatu katika shambulio la IS

Askari watatu wa Uturuki wameuawa Jumanne hii kaskazini mwa Syria katika shambulizi la kwanza baya kabisa kuhusishwa kundi la Islamic State (IS) tangu kuanza kwa mashambulizi ya Uturuki wiki mbili zilizopita, kwa mujibu wa vyanzo rasmi.

Vifaru vya Uturuki nje kidogo ya mji wa Syria wa Jarablus, Septemba 2, 2016
Vifaru vya Uturuki nje kidogo ya mji wa Syria wa Jarablus, Septemba 2, 2016 AFP
Matangazo ya kibiashara

Operesheni kababme iliyozindua Agosti 24, inalenga kulitimua kundi la Is na wanamgambo wa Kikurdi kwenye mpaka wake. Shambulizi la Jumanne hii pia limewajeruhi askari watano wa Uturuki, vyanzo hivyo vimeendelea kusema.

"Watatu miongoni mwa ndugu zetu wamekufa mashujaa na watano wamejeruhiwa katika shambulio la roketilililoendeshwa na kundi la Islamic State dhidi ya magari yetu mawili ya kijeshi,"jeshi limetangaza katika taarifa yake, likinukuliwa na runinga binafsi ya NTV.

Afisa mwandamizi wa Uturuki athibitisha idadi hiyo ya vifo.

Ni kwa mara ya kwanza jeshi la Uturuki linapoteza watu wake, ambapo kundi la Islamic State linahusishwa tangu kuanza kwa operesheni hiyo. Agosti 28, Uturuki ilitangaza kifo cha mmoja wa askari wake, ikiwashtumu wanamgambo wa Kikurdi kuwa chanzo.

Jeshi limesema shambulizi hili liliendeshwa kusini mwa mji wa Al-Rai, karibu na mpaka, ambapo vifaru vya Uturuki vilizindua mapigano mapya mwishoni mwa juma lililopita.