UTURUKI-USALAMA

Ndugu wa Fethullah Gulen akamatwa Uturuki

Mtu aliyejifunika bendera ya Uturuki akipita mbele ya gari ya kijeshi karibu na uwanja wa ndege mjini Istanbul Julai 16 2016, kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotibuliwa.
Mtu aliyejifunika bendera ya Uturuki akipita mbele ya gari ya kijeshi karibu na uwanja wa ndege mjini Istanbul Julai 16 2016, kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotibuliwa. REUTERS/Baz Ratner

Polisi nchini Uturuki imemkamata ndugu wa mhubiri wa zamani Fethullah Gulen ambaye anatuhumiwa kuongoza jaribio la mapinduzi Julai 15, shirika la habari la linalounga mkono serikali la Anadolu limetangaza Jumapili hii Oktoba 2.

Matangazo ya kibiashara

Kutbettin Gulen, ndugu wa kwanza wa mhubiri wa zamani amekamatwa nyumbani kwa mmoja wa ndugu zake katika mji wa Izmir, wilayani Gaziemir, magharibi mwa nchi, chanzo hicho kimesema.

Kwa upande wa rais Uturuki amesema hakuna shaka, chanzo cha maovu yote ya Uturuki ya leo ni kutokana na mshauri wake wa zamani na mfadhili Fethullah Gulen. Kwa kuamini hoja yake,Rais Erdogan amesema Fettulah Gulen anahusika katika jaribio la mapinduzi la mwezi Julai.

Lakini Fethullah Gullen anaishi nchini Marekani na kwa sasa Washington haina nia ya kumrudisha nchini mwake, Uturuki. Hata hivyo ndugu na dada zake bado wanaishi nchini Uturuki ikiwa ni pamoja na Kutbettin Gulen. Kutbettin Gulenamekamatwa ili ahojiwe. Anashtumiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi lenye silaha. Wipwa wawili wa Fethullah Gulen walikabiliwa na hali kama hiyo miezi miwili iliyopita.

Kwa amri ya rais wa Uituruki tayari watu 32,000 wametupwa jela. Maafisa wa elimu, polisi au vyombo vya sheria, jeshi, wanachama wa vyama vya kiraia na hata waandishi wa habari wamewekwa jela. Hakuna tarehe ambayo imetangazwa kwa ajili ya kesi yao kusikilizwa. Hata hivyo, serikali ya Uturuki imeamua kuwaachilia huru wafungwa 38,000ili kuwapa nafasi wafungwa wapya.