THAILAND-HAKI ZA BINADAMU

Mwanaharakati wa Hong Kong Joshua Wong akamatwa Thailand

Mwaka jana, Joshua Wong alikuwa amepigwa marufuku kuingia nchi jirani ya Malaysia, serikali ilimrejeshaa Hong Kong.
Mwaka jana, Joshua Wong alikuwa amepigwa marufuku kuingia nchi jirani ya Malaysia, serikali ilimrejeshaa Hong Kong. REUTERS/Bobby Yip

Mmoja wa viongozi wa mashirika yanayounga mkono demokrasia nchini Hong Kong, Joshua Wong, alikamatwa na kuwekwa kizuizini Jumanne wiki hii alipowasili nchini Thailand.

Matangazo ya kibiashara

Joshua Wong Alikuwa alikuja kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya mwaka 1976 mjini Bangkok. Joshua Wong anatazamiwa kurejeshwa Hong Kong katika masaa yajayo.

Angelikuwa mgeni wa heshima katika Chuo Kikuu cha Chulalongkorn mjini Bangkok. Joshua Wong angelihutubia Alhamisi wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka arobaini ya mauaji ya wanafunzi, waliouawa na polisi ya Thailand na makundi ya mrengo wa kulia mwaka 1976.

Lakini mara tu ya kushuka kutoka ndani ya ndege, polisi ilimkamata na kumuweka kizuizini kwa ombi la serikali ya China. Wakati ambapo mashirika ya haki za binadamu yana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kusafirishwa hadi mjini Beijing, polisi ya Thailand kwa upande wake, imesema atasafirishwa Hong Kong.

Joshua Wong alikuwa mmoja wa viongozi wa kuu wa mapinduzi yayaliyojulikana kwa jina la 'mapinduzi ya miavuli'.

kukamatwa na kufukuzwa kwa Joshua Wong kunathibitisha uzito muhimu wa China juu ya maamuzi ya serikali ya kijeshi ya Thailand.