UFILIPINO-SIASA

Duterte: Mungu amenionya kutorudi kutumia lugha chafu

Rais wa Ufilipino Rodrigo Dulerte.
Rais wa Ufilipino Rodrigo Dulerte. REUTERS/Lean Daval Jr.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, ametoa ahidi ya kuacha kutumia lugha chafu hasa matusi dhidi ya watu mbalimbali baada ya kile anachosema kuwa alipata ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu ulimuonya kutorudi kutumia lugha hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Rais Rodrigo Dulerte alimtusi Rais Barack Obama kuwa ni"mwana wa kahaba" na huku akieleza kuwa kiongozi huyo wa Marekani ni sawa na "shetani".

Bwa Dulerte amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupata ufunuo alipokuwa safarini akitokea nchini Japan.

Rodrigo Dulerte amewatusi watu mashuhuri mbalimbali

Rais wa Ufilipino alimtusi Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry kwa kumuita "mwendawazimu".

Itafahamika kwamab nchi ya Ufilipino ina Wakatoliki wengi barani Asia.

Bw Dulerte alimwita kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis kuwa ni "mwana wa kahaba"

Alimwita pia balozi wa Marekani nchini Ufilipino kuwa ni "mwana wa kahaba na ni mpenzi wa jinsia moja".

Bw Duterte amesema alipata ujumbe kutoka kwa Mungu alipokuwa kwenye ndege, na watu wengine ambao karibu wote walikuwa wamelala, huku akisikia sauti ikimuonya: nitaiangusha ndege hii, usipojirekebisha.

Amesema sauti hiyo ilijitambulisha kusema kuwa ni ya Mungu.

Bw Dulerte amesema atatekeleza ujumbe huo kutoka kwa Mungu, kwani ahadi ya Mungu ni sawa na ahadi kwa raia wa Ufilipino.