PAKISTAN-USALAMA

Polisi yajiandaa kwa wiki ya maandamano mjini Islamabad

Kiongozi wa upinzani nchini Pakistani, Imran Khan,  akiongea na vyombo vya habari mjini Islamabad, Oktoba 28, 2016.
Kiongozi wa upinzani nchini Pakistani, Imran Khan, akiongea na vyombo vya habari mjini Islamabad, Oktoba 28, 2016. REUTERS/Stringer

Tangu Alhamisi usiku, polisi imewakamata wafuasi kadhaa wa chama cha upinzani cha PTI. Chama hiki kimepangaa kuzuia mji mkuu wa Pakistan kuanzia Jumatano kwa kumpindua Waziri Mkuu anayeshtumiwa na chama hiki kujihusisha na rushwa.

Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, mahakama ilipiga marufuku mikusanyiko yoyote ile na maandamano katika mji wa Islamabad kwa kuepuka kuzuka kwa vurugu katika mji mkuu wa nchi hiyo kufuatia maandamano yaliyotangazwa na chama cha PTI kuanzia Jumatano Novemba 2.

Siku ya Alhamisi jioni, polisi waliwaweka mbaroni wafuasi arobaini wa chama hiki kikuu cha upinzani, walipokutana kwa ajili ya kusanyiko la vijana. Chama cha PTI (Pakistan Tehreek-e-Insaf), wanataraji kuhamasisha wakazi wa mji wa Islamabad kusalia nyumbani ili kumshinikiza Waziri Mkuu Nawaz Sharif, anayehusishwa katika kesi ya Panama Papers kwenye orodha ya watu wanoongoza rushwa, kujiuzulu.

kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika chama cha PTIbingwa wa zamani wa kriketi Imran Khan, amekua akiwahamasisha kila siku wafuasi wake kwa tarehe ya mwisho ya Jumatano hii. Vikosi vya usalamavimepiga kambi kwenye makazi yake, karibu na mji wa Islamabad, ambapo watu kadaa walikamatwa pamoja na silaha za kivita.

Barabara kadhaa zinazoingia katika mji wa Islamabad zimefungwa kwa siku nzima ya Jumapili hii, serikali inatiwa hofu na kuwasili kwa wafuasi wengi wachama cha PTI, ambao tayari walikwamisha shughuli katika mji mkuu wa Pakistani kwa muda wa miezi minne mwaka 2014.