AMNESTY-URUSI

Amnesty International yatupwa barabarani nchini Urusi

Jumatano hii viongozi wa mji wa Moscow walichukua ghafla uamuzi wa kufunga makao makuu ya shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty Internatinal mjini Moscow bila kuwataarifu wahusika.

Amnesty international yafungiwa makao makuu yake nchini Urusi.
Amnesty international yafungiwa makao makuu yake nchini Urusi. Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea siku moja baada ya shirika hili kiutoa wito wa kufanya uchunguzi kuhusu mateso yanayomkabili gerezani Ilya Dadine, mwanaharakati wa upinzani na wa kwanza kuhukumiwa chini ya kifungu cha sheria ya hivi karibuni juu ya uvunjaji wa sheria kuhusu maandamano.

Wafanyakazi wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International walipowasili mapema asubuhi mbele ya ofisi walikuta kufuli zilibadilishwa na muhuri uliwekwa kwenye mlango na viongozi wa manispaa la jiji la Moscow, na 'kupigwa marufuku kuingia katika ofisi zao bila kuwepo kiongozi wa mji wa Moscow, ' mmiliki wa jengo hilo ambalo ni makao makuu ya amnesty International nchini Urusi. Namba ya simu iliandikwa kwa mkono ili kuwasiliana na kiongozi huyo.

"Katika saa za mwanzo, tulijaribu kuelewa nini kilichotokea, tlipiga simu kwa namba tuliyopewa, lakini hakuna aliyepokea," Ivan Kondratenko, mmoja wa wafanyakazi wa Amnesty International ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyokiongozi wa manispaa ya jiji la Moscow alitoa tangazo kwenye vyombo vya habari akieleza kuwa Amnesty International, ingawa walipewa taarifa mara kadhaa, walikua bado hawajalipa kodi. "Uongo mtupu," amesema Kondratenko. Kamwe hatujapokea taarifa yoyote ya malimbikizo ya malipo,  " amesema Kondratenko. Kwa mujibu wa Kondratenko, Amnesty International imelipwa bili zote kwa miaka ishirini ambapo inakodi jengo hilo lenye mita 60 mraba katikati mwa mji wa Moscow.

"Wakala wa nchi za kigeni"

"Hatujui sababu zilizopelekea viongozi wa mji wa Moscow kuwakatalia wafanyakazi wetu kuingia katika ofisi zetu, kwa upande wake amesema John Dalhuisen, mkurugenzi wa Amnesty International barani Ulaya, lakini kutokana na hali ya sasa kwa mashirika ya kiraia nchini Urusi, kuna uwezekano mkubwa kuwa ndio sababu ya uamuzi huo. " Kwa kweli, hatua zimeendelea kuchukuliwa dhidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali, hasa yale ya kutetea haki za binadamu, yanayotuhumiwa na serikali ya Urusi kwamba ni vyombo vya nchi za Magharibi vyenye nia ya kudhoofisha kutoka ndani ya Urusi. Tangu mwaka 2012, sheria inaamuru mashirika yanayopokea fedha kutoka ugenini kujiandikisha kama 'mawakala wa nchi za kigeni.'

Wakati ambapo Amnesty International mara kwa mara imekua ikishtumu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Urusi, 'ishara' hii inatumwa kwa shirika hili baada ya kutoa wito wa kufanya uchunguzi kuhusu mateso anayoyapata gerezani Ilya Dadine, mwanaharakati wa upinzani na mtu wa kwanza kukutwa na hatia chini ya sheria ya hivi karibuni juu ya uvunjaji wa sheria ihusuyo maandamano. Aliandamana peke yake akiwa na bango lililoandikwa 'mimi ni Charlie.'