UTURUKI-USALAMA-SIASA

Uturuki: chama kikuu kinachounga mkono Wakurdi chajiondoa bungeni

Chama kikuu kinachowaunga mkono Wakurdi, ambapo wajumbe wake, ikiwa ni pamoja na wabunge na viongozi wawili kutoka chama hiki walikamatwa siku ya Jumapili, kimetangaza kujiondoa katika shughuli zote za Bunge, ili kupinga dhidi ya ukandamizaji unaoendelea kupanda kwa kiwango cha juu.

Sebahat Tuncel, mbunge na rais mwenza wa chama cha HDP, aliyeikamatwa wakati wa maandamano ya upinzani anazuiliwa kwa kusubiri kesi.
Sebahat Tuncel, mbunge na rais mwenza wa chama cha HDP, aliyeikamatwa wakati wa maandamano ya upinzani anazuiliwa kwa kusubiri kesi. REUTERS/Sertac Kayar
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Peoples Democratic Party (HDP), chama cha tatu nchini, chenye wabunge 59,hakitoshiriki vikao vya bunge wala shughuli za tume, chama hicho kimesema katika taarifa yake.

Wabunge ambao hawakukamatwa watajishughulisha kwa kukutana na wapiga kura wao, wakifanya zoezi la "nyumba kwa nyumba, kijiji kwa kijiji na wilaya kwa wilaya" na kisha kutoa mapendekezo juu ya jinsi chama chao kinaweza kuendelea na shughuli zake.

Wabunge tisa, ikiwa ni pamoja viongozi wawili wa chama cha HDP, Selahattin Demirtaş na Bibi Figen Yüksekdag waliwekwa rasmi kizuizini Ijumaa Novemba 4 kwa kusubiri kesi. Wanatuhumiwa kuwa na uhusiano au kushirikiana na vuguvgu la PKK.

Chama cha HDP kimekua kikikanusha vikali kuwa hakina uhusiano wowote wa kisiasa na vuguvugu la PKK, ambalo kwa kwa miongo mitatu limeendelea na mapambano ya silaha kwa madai ya haki zaidi na uhuru kwa Wakurdi.