UFILIPINO-MAREKANI-USHIRIKIANO

Serikali ya Ufilipino kutonunua silaha kutoka Marekani

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, amesema nchi yake haina haja tena ya kununua silaha kutoka nchini Marekani, huku akiongeza kuwa ameagiza kufutiliwa mbali kandarasi ya kununua maelfu ya bunduki kutoka nchini humo.

RAis wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema nchi yake imevunja mkataba wa kununua silaha kutoka Marekani..
RAis wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema nchi yake imevunja mkataba wa kununua silaha kutoka Marekani.. REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Idara ya polisi ya Ufilipino ilikuwa imepangiwa kununua takriban bunduki 26,000 kutoka Marekani.

Kumekuwepo taarifa kwamba Marekani ilikuwa imepanga kutoiuzia Ufilipino silaha hizo, kutokana na wasiwasi kuhusu ukatili wa Rais wa nchi hiyo Rodrigo Duterte hasa katika kukabiliana na walanguzi wa madawa ya kulevya.

Hata hivyo Rais Rodrigo Duterte amesema kuwa taifa lake litatafuta njia mbadala ya kununua silaha hizo kwingine kwa bei nafuu.

Uhusiano baina ya Marekani na Ufilipino, nchini ambazo zilikuwa washirika kwa muda mrefu, umeingiliwa dosari tangu Rodrigo Duterte achukuwe hatamu ya uongozi wa nchi.