BURMA-USALAMA

Jeshi la Burma ladai kuwaua waasi 28 magharibi mwa nchi

Jeshi la Burm alimehakikisha kuwa limewaua Jumapili hii waasi 28 katika mapigano mapya yaliyozuka katika jimbo la Rakhine, magharibi mwa Burma ambapo, kwa mujibu wa serikali, makundi ya Waislamu wenye msimamo mkali yanaendesha harakati zao.

Picha hii imetolewa na majeshi ya Burma Novemba 13, 2016, ikionyesha shimbo baada ya mlipuko wa bomu karibu na kijiji cha Maungdaw, katika jimbo la Rakhinekaribu na mpaka na Bangladesh.
Picha hii imetolewa na majeshi ya Burma Novemba 13, 2016, ikionyesha shimbo baada ya mlipuko wa bomu karibu na kijiji cha Maungdaw, katika jimbo la Rakhinekaribu na mpaka na Bangladesh. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kwa jumla watu 28 wameuawa," kutoka upande wa waasi ambao walishambuliwa askari na polisi wakati wa operesheni iliyoendeshwa katika jimbo la mpakani la Bangladesh, taarfa ya jeshi imetangaza.

Jeshi halijataja idadi ya waathirika upande wa vikosi vya usalama na ulinzi.

Yote yalianza wakati wauaji walishambulia kundi la askari polisi na wanajeshi waliokuwa wamekuja Jumapili hii asubuhi kufanya ukaguzi kijiji ambapo nyumba hamsini zilichomwa moto siku moja kabla.

"Wauaji saba walishambulia askari, ambao walijibu. Washambuliaji sita waliuawa," jeshi limehakikisha.

Katika kijiji cha pili kilichokaguliwa wakati wa mchana, "wakati huo waasi 20 wakiwa na silaha wawalishambulia" na "washambuliaji 19 waliuawa," jeshi limeomngeza,huku likibaini kwamba lilipata miili mingine mitatu katika kijiji jirani baada ya makabiliano.

Mapigano hayo yanajiongeza kwa mfululizo wa mashambulizi kwenye vituo vya polisi kwenye mpaka na Bangladesh mapema mwezi Oktoba, ambapo polisi tisa waliuawa.

Kwa uchache watu 29 waliuawa na vikosi vya usalama katika operesheni kabambe ya kijeshi.

Machafuko haya yanatia hofu ya kutokea kwa mapigano ya kikabila ya mara kwa mara kama yale ya mwaka 2012 kati ya Waislamu na Mabudha yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na mamia ya maelfu kuyahama makazi yao.

Tangu wakati huo, zaidi ya watu 100,000 kutoka jamii ya Rohingyas wamekusanyika katika makambi ya wakimbizi. Baada ya kuchukuliwa kama wahamiaji haramu kutoka Bangladesh, watu hawa hawapati huduma yoyote, katika soko la ajira, shule kwa watoto na hawana uhuru wa kutembea.

Hali hii ya kuyumba kwa usalama ni changamoto kwa Aung San Suu Kyi na serikali yake, ambayo ni ya kwanza ya kiraia nchini Burma kwa miongo kadhaa.

Baada ya mashambulizi ya Oktoba, Rais wa Burma, Htin Kyaw, mshirika wa karibu wa Aung San Suu Kyi, aliwanyooshea kidole cha lawama "wanajihadi" kutoka kundi lisilojulikana hadi sasa, Aqa Mul Mujahidin, akihakikisha kwamba kiongozi wake alipewa mafunzo na wapiganaji wa kundi la Taliban kutoka Pakistan na linasaidiwa kifedha na makundi ya Mashariki ya Kati.

Pia alilishtumu kundi hili kutoa mafunzo katika jimbo la Rakhine State na kuendeleza "itikadi ya msimamo mkali miongoni mwa Waislamu wa jimbo hilo."