UTURUKI-EU

Rais Erdogan apangilia kura ya maoni juu ya Uturuki kwa EU

Rais wa Turuki Recep Tayyip Erdogan ameonya Umoja wa Ulaya Jumatatu Novemba 14, akitishia kupiga kura ya maoni mwaka 2017kuhusu kuendelea au la na mazungumzo juu ya Uturuki kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, mchakato ambayo ulianza miaka kumi na miwili iliyopita.

Uturuki ni mgombea kwenye uanachama wa Umoja wa Ulaya.
Uturuki ni mgombea kwenye uanachama wa Umoja wa Ulaya. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Uhusiano tayari umeingiliwa kasoro kati ya Ankara na Brussels, hasa kwa sababu ya kukataa kwa Umoja wa Ulaya kutoa visa kwa raia wa Uturuki kwa ajili ya kupatiwa utekelezaji wa makubaliano ya wakimbizi nchini Uturuki.

Baada Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, labda uamuzi unaofuata ni wa Uturuki kufutilia mbali mchakato wa kujiunga na Umoja huo. Bila shaka, Uturuki si mwanachama wa Umoja wa Ulaya, lakini Rais Erdogan alizungumzia mara mbili katika siku za hivi karibuni hoja ya Uturuki kuamua kupitia kura ya maoni.

Kwa mujibu wa rais Uturuki, ni njia ya kuweka shinikizo kwa Ubelgiji na ikiwezekanakusitisha mara moja mchakato huo kupitia kura ya maoni. Utawala wa Recep Tayyip Erdogan unakabiliwa namvutano na Ulaya tangu, hasa kushindwa kwa mapinduzi.

Hoja ya kura ya maoni

Uamuzi wa Uturuki kuachana na mchakato wa kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya utasababisha madhara makubwa. Uturuki inapata zaidi ya Euro bilioni moja kwa mwaka kama msaada kutoka Umoja wa Ulaya, kwa nchi inayowania nafasi hiyo.