Trump na Putin wanapangilia "kuweka sawa" mahusiano kati ya Urusi na Marekani

Donald Trump alizungumza na Vladimiri Putin kwa mara ya kwanza kwa njia ya simu tangu achaguliwe, Novemba 14, 2016.
Donald Trump alizungumza na Vladimiri Putin kwa mara ya kwanza kwa njia ya simu tangu achaguliwe, Novemba 14, 2016. REUTERS/Carlo Allegri

Rais wa Urusi na rais mpya mteule wa Marekani walifanya mazungumzo kwa njia ya simu siku ya Jumatatu Novemba 14. Mazungumzo ya kwanza tangu ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa urais wa Novemba 8, 2016. Ikulu ya Urusi (Kremlin) ilitangaza kuwa wamekubaliana "kurejesha" uhusiano kati ya nchi zao mbili.

Matangazo ya kibiashara

Katika mazungumzo kwa njia ya simu, wawili hao waliamua 'kwa makubaliano ya pamoja' kwa mujibu wa Kremlin, Vladimir Putin alimpongeza kwa mara nyingine tena Donald Trump kwa ushindi wake na alisema yuko 'tayari kuanzisha mazungumzo na utawala mpya wa Donald Trump kuhusu usawa, kwa mujibu wa kanuni ya kuheshimiana na bila ya mmoja kuingilia katika masuala ya ndani ya mwingine. '

Donald Trump na Vladimir Putin wamebaini kwa pamoja kuwa uhusiano kati ya Marekani na Urusi si mzuri na walitangaza kushirikiana kwa pamoja kwa kuewka sawa mahusiano kati ya nchi hizi mbuli, kwa mujibu wa Kremlin.

Ni mazungumzo ya kwanza kwa njia ya simu kati ya wawili hao tangu kuchaguliwa kwa Donald Trump, hata kama rais wa Urusi alituma ujumbe wa kumpongeza Donald Trump.

Wakati wa harakati zake za kampeni, Trump aliendelea kumpongeza rais huyo wa Urusi, akimuelezea kama mtu mwenye upeo mkubwa ukimlinganisha na rais anayeondoka madarakani Barack Obama.