UT-SHERIA-JAMII

Serikali ya Uturuki yarejesha nyuma muswada tata kuhusu ubakaji

Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim mbele ya Bunge la Uturuki, Novemba 8, 2016.
Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim mbele ya Bunge la Uturuki, Novemba 8, 2016. REUTERS/Umit Bektas

Serikali ya Uturuki imeamua kurejesha nyuma muswada wenye utata, ambao ulikua ukipanga kusimamishwa kwa madai ya unyanyasaji wa kijinsia wakati mhusika atafunga ndoa na mwathirika wake.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildrim ameondoa mswada ambao unawasamehe wanaume waliowabaka wasichana wadogo iwapo wamewaoa.

Mswada huo ambao ulifanyiwa marekebisho ulirudishwa saa kadhaa kabla ya kupigiwa kura bungeni.

Kwa mujibu wa serikali ya Uturuki nakala hii ilikuwa inalenga kulinda familia kutoka ndoa za utotoni. Hata hivyo Waziri Mkuu wa Uturuki ametangaza Jumanne hii Novemba 22 kwamba muswada huo haukufutwa, lakini umefanyiwa marekebisho.

Serikali ya Uturuki ilikua imewasilisha muswada huu kama jibu kwa ndoa za utotoni, ambazo zimekithiri katika baadhi ya maeneo. Kwani mahusiano ya kimapenzi na watoto walio na umri wa chini ya miaka 16 yanapigwa marufuku na sheria, wanaume wamekua wakipatikana na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia, hata kama wote wawili wameridhiana kufanya kitendo hicho.

Hoja hii ilitolewa na chama madarakani cha AKP katika siku za hivi karibuni. Chama hiki kimekua kikibaini kwamba wanawake waliobakwa na watoto wao walikua wakitengwa wakati mume yuko jela. Lakini mitokana na maandamano makubwa dhidi ya muswada huo, serikali imeamua kuurejesha nyuma. Hata ndani ya chama tawala, wafuasi wengi wamekua wakipinga dhidi ya muswada huo.

Mswada huo utarudishwa katika tume ambayo itachukua maoni ya upinzani na mashirika ya kijamii, amesema Bw. Yildirim.

Hii itaruhusu makubaliano na kutoa muda kwa upinzani kuwasilisha mapendekezo yake.