CHINA-MAREKANI-USHIRIKIANO

China: tuko tayari kuirejesha manuwari ya Marekani

Eneo la bahari la Zhanjiang, mkoani Guangdong, nchini China, Septemba 19, 2016.
Eneo la bahari la Zhanjiang, mkoani Guangdong, nchini China, Septemba 19, 2016. REUTERS/Stringer

Wizara ya ulinzi ya Marekani imebaini kwamba kuwa imekubaliana na China kuwa itairejesha manuwari ya Marekni iliopatikana katika bahari ya kusini mwa China. China iliikamata manuwari hiyo katika maji ya kimataifa Alhamisi Desemba 15.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kuwa manuwari hiyo inayojulikana kama UUV ilikuwa ikitumika kubeba utafiti wa kisayansi wakati ilipokamatwa na kutaka irejeshwe mara moja.

Marekani kupitia wizara yake ya ulinzi imeionya China kutochukua hatua kama hiyo katika siku zijazo.

China haijasema sababu zilizopelekea inachukua hatua hiyo na kuishutumu Marekani kwa kulifanya jambo hilo kuwa kubwa.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump aliandika katika mtandao wake Twitter., akisema kuwa ameishutumu China kwa kuiiba meli hiyo. “ Tunafaa kuielezea China kusalia na manuwari hiyo walioiba, " Rais Mteule wa Marekani Donadl Trump amesema.”

Kisa hicho ni miongoni mwa visa vibaya zaidi vya makabiliano ya kijeshi kati ya mataifa hayo yenye uwezo mkubwa wa kijeshi katika kipindi cha miongo kadhaa.