CHINA-USALAMA

China kuanzisha operesheni za kijeshi katika bahari ya Pasifiki

Chombo cha kwanza cha kikosi cha majini cha China, Liaoning, kilichopigwa picha katika mji wa Daliantarehe 6 Julai 2014.
Chombo cha kwanza cha kikosi cha majini cha China, Liaoning, kilichopigwa picha katika mji wa Daliantarehe 6 Julai 2014. CHINA OUT AFP PHOTO

China ilitangaza Jumamosi hii Desemba 24 kwamba itapeleka kwa mara ya kwanza katika bahari ya Pacifiki magharibi chombo chake cha kijeshi kwa operesheni za kijeshi. Kupelekwa kwa chombo hiki cha China kijulikanacho kwa jina la Liaoningg katika eneo hilo ni mara ya kwanza. Mazoezi haya yanakuja wakati ambapo mvutano uliibuka kati ya Beijing na Taiwan.

Matangazo ya kibiashara

Katika hatua hii, haijajulikana operesheni hizi za kijeshi katika eneo hilo la bahari zitachukua muda wa kiasi gani na njia itakayotumiwa kwa chombo hiki. Chombo hiki ambacho kinatumiwa kwa kubeba na kutwa kwa ndege kinapiga kambi mjini Dalian, kaskazini mwa China, kitaingia katika bahari ya Pacifiki kupitia kisiwa kisiwa kinachotenganisha Taiwan na kusini mwa Japan.

Wizara ya Ulinzi ya Japan imesema kimeona chombo kikubwa, kikiwa kimebeba vifaa mbalimbali vya kijeshi.

Operesheni hii inakwenda sambamba na kuibuka kwa mvutano kati ya Taiwan na Beijing uliyotokana na kauli za uchochezi za rais mteule wa Marekani Donald Trump ambaye alisema hafurahii sera ya kujiunga kwa "China moja."

Jeshi la China, linalotafuta kujiimarisha, limelizidisha mazoezi ya kijeshi ili kukabiliana na kikosi cha majini cha Marekanii. Kikosi cha majini cha marekani ndio pekee kinachoonekana chenye nguvu katika bahari ya Pasifiki, hali ambayo inazidi kuikera Beijing.