URUSI-AJALI

Urusi: kisanduku cheusi cha pili cha Tupolev Tu- 154 chapatikana

Bahari Nyeusi mjini Sochi, ambapo ndege ya kijeshi ya Urus Tupolev Tu-154 ilianguka.
Bahari Nyeusi mjini Sochi, ambapo ndege ya kijeshi ya Urus Tupolev Tu-154 ilianguka. REUTERS/Maxim Shemetov

Wizara ya Ulinzi ya Urusi iimetangaza kuwa timu za uokoaji zilipata kisanduku cheusi cha pili cha ndege ya kijesi ya Urusi iliyoangika katika bahari Nyeusi siku ya Jumapili jioni, na kuua watu tisini na wawili waliokua katika ndege hiyo iliyokua ikielekea nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi miili kadhaa ya watu waliokua katika ndege hiyo aina ya Tupolev Tu-154 pia ilipatiakana katika eneo la ajali katika pwani ya Sochi, na imelipelekwa mjini Moscow kwa ajili ya kuitambua.

Kisanduku kingine cheusi kilipatikana Jumanne wiki hii na kwa sasa kinafanyiwa uchunguzi.

Vipande kadhaa vya ndege hiyo iliyoanguka viligunduliwa na watu 3,500 waliokua wakitumika mchana na usiku katika eneo la tukio baada ya kutumwa na serikali.

Serikali inaonekana kuwa tayari imetupilia hoja ya shambulizi kama sababu ya ajali ya Tupolev Tu-154, iliyotokea Jumapili jioni baada ya kuruka kutoka mi wa Sochi (kusini mwa Urusi) ikielekea Syria, ikiwa na watu 92 ikiwemo bendi ya wanamuziki 60 wa jeshi la Urusi.