URUSI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Wanadiplomasia wa urusi wameondoka nchini Marekani

Msafara wa magari ya wanadiplomasia wa Urusi ukiondoka katika kituo kinachomilikiwa na Urusi katikati mwa mji wa Maryland.
Msafara wa magari ya wanadiplomasia wa Urusi ukiondoka katika kituo kinachomilikiwa na Urusi katikati mwa mji wa Maryland. REUTERS / Joel Schectman

Wanadiplomasia wa Urusi waliofukuzwa kwa amri ya Rais Barack Obama waliondoka Jumapili hii Januari 1 mjini Washington, mashirika ya habari ya Urusi yamearifu yalinukuu ubalozii wa Urusi.

Matangazo ya kibiashara

"Ndege waliokuwemo iliondoka. Kwa kweli wote waliondoka," Idara ya mawasiliano ya ubalozi wa Urusi imetangaza ikinukuliwa na shirika la habari la RIA.

Siku ya Alhamisi Barack Obama aliamuru kuwafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi katika miji ya Washington na San Francisco na kufunga vituo viwili vya Urusi katika miji ya New York na Maryland, katika kukabiliana na kile White House ilikiita kama kampeni ya mashambulizi ya kompyuta ya Urusi dhidi ya taasisi na viongozi wa kisiasa wa Marekani wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2016.

Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Ijumaa aliamua kutomfukuza mwanadiplomasia yeyote wa Marekani katika kukabiliana na hatua hizo, akisema kuwa anasubiri Donald Trump kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi ili kuchukua uamuzi juu ya mustakabali wa mahusiano kati ya nchi hizi mbili.