UTURUKI-USALAMA

Watu 39 wauawa mjini Istanbul

Mwaka mpya washerehekewa kwa majonzi nchini Uturuki.
Mwaka mpya washerehekewa kwa majonzi nchini Uturuki. YASIN AKGUL / AFP

Watu wasiopungua 39 waliuawa na sitini kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya klabu ya burudani maarufu mjini Istanbul, la Reina. Shambulio hili lilitokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, Januari 1,Waziri wa Mambo ya ndani alitangaza Jumapili hii asubuhi. Hilii ni shambulio la sita kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji hajulikani aliko na hakina kundi ambalo limedai mkuhusika na shambulio hilo wakati ambapo rais Erdogan amesisitiza kuwa serikali ya Uturuki bado inashikilia uamuzi wa kukabiuliana na vitisho hivyo.

Baraza la usalama lilikuta wakati wa mchana mjini Istanbul chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Binali Yildirim lakini kwenye mitandao ya kijamii na katika vyombo vya habari, maswali tayari yameibuka: watu wamekua wakijiuliza, jinsi shambuliaji aliyeweza kuingia na silaha, katika klabu ya burudani maarufu kwa kudhibiti wateja wake. Swali jingine linalozua utata, hoja ya makundi mbalimbali ya Kiislam na pia, magazeti yenye itikadi za kidini ambayo yaliwatolea wito wananchi wa Uturuki lutosherehekea Januri 1, Sikuukuu ambayo haiendani sambamba na Uislamu. Wakati huo huo gazeti la kila siku la Milli lilichapisha habari Jumamosi yenye kichwa cha habari: mssherehekei Mwaka Mpya, hili ni onyo la mwisho.

Kwa mujibu wa Rais Erdogan, katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya rais, shambulio hili lilikuwa linalenga "kuchochea machafuko nchini" lakini "kama taifa, tutapambana hadi mwisho sio tu mashambulizi ya makundi ya kigaidi yenye silaha na vikosi vinavyoshirikiana na makundi hayo, lakini pia mashambulizi yao ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, " Erdogan amewahakikishia wananchi wake.

"Uturuki inapambana dhidi ya makundi ya kigaidi yanayoendesha harakati zao katika nchini humo, dhidi ya magaidi wa Fethullah Gulen, pia dhidi ya makundi yenye mafungamano na IS nchini Syria na Iraq, amebaini Waziri Mkuu Binali Yildirim. Bila shaka, tunajua kwamba kutakuwa na ulipizaji kisasi, lakini tutakabiliana na ugaidi huo."

Idadi ya watu waliouawa katika shambulio hilo iliongezeka Jumapili asubuhi ahdi kufiki 39. Wageni ni miongoni mwa watu waliouawa. Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, raia wa kigeni ni miongoni mwa waliouawa. Aidha watu 69 walijeruhiwa ikiwa ni pamoja na wanne ambao wako katika hali mbaya.