UTURUKI-IS

Kundi la IS lakiri kuhusika katika shambulio la Istanbul

Kundi la Islamic State, limekiri kuhusika kwenye shambulio lililotekelezwa katika klabu moja ya usiku jijini Instanbul, Uturuki, wakati wa sherehe za kuamkia mwaka mpya, ambapo watu 39 waliuawa.

Askari wa Uturuki wakipiga doria jirani na eneo lilipotekelezwa shambulio katika klabu ya usiku. 1 januari 2017
Askari wa Uturuki wakipiga doria jirani na eneo lilipotekelezwa shambulio katika klabu ya usiku. 1 januari 2017 Turkish police stand guard outisde the Reina nightclub by the Bo
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake iliyosambazwa kupitia mitandao ya kijamii, wanajihadi hao wamesema kuwa "mwanajeshi wetu" ametekeleza shambulio kwenye klabu ya usiku ua Reina.

Taarifa ya kundi hilo imeongeza kuwa mpiganaji wake aliyetekeleza shambulio, alitumia bomu la kutupa kwa mkono pamoja na bunduki.

Kundi hilo linautuhumu utawala wa Uturuki, ambao kwa sehemu kuwa unaongozwa kwa misingi ya dini ya kiislamu, kuwa inatetea ukristo, wakihusisha na uamuzi wa nchi hiyo kushirikiana na washirika wake kuliangamiza kundi hilo.

Taarifa ya kundi hilo imeongeza kuwa, shambulizi walilotekeleza ni kutokana na hatua ya Uturuki kushiriki kwenye vita dhidi ya kundi hilo nchini Syria.

Uturuki inawaunga mkono upinzani nchini Syria, lakini pia imeanzisha vita yake na wapiganaji wa Islamic State nchini Syria toka mwezi Agosti mwaka jana.

Mashambulizi mfululizo yameshuhudiwa nchini Uturuki katika mwaka 2016, huku baadhi ya mashambulizi yakidaiwa kitekelezwa na wapiganaji wa Kikurdi.