Vita vya maeneno vyaibuka kati ya Trump na Korea Kaskazini
Imechapishwa:
Korea Kaskazini inasema tamko la rais mteule wa Marekani Donald Trump kuwa Korea Kaskazini haina uwezo wa kutumia silaha zake za masafa marefu, ni onyo tosha kwa serikali ya Pyongyang.
Kauli ya Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter, ilikuja baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un kusema kuwa nchi yake ipo katika maandalizi ya lala salama kutengeza silaha za kisasa za masafa marefu na kuimarisha uimara wa silaha zake.
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, alipuuzilia mbali madai ya Korea Kaskazini kuwa imeunda Kombora linaloweza kuwasilisha zana za nuklia hadi Marekani.
Bwana Trump aligusia maneno ya kujigamba ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ujumbe wake wa mwaka mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia hatua ya mwisho
Donald Trump ameshutumu China kwa kushindwa kuthibiti mshirika wake Korea Kaskazini na pia akalaumu Beijing kwa kupokea kiasi kikubwa cha pesa na mali kutoka Marekani.