CHINA-MAREKANI-TAIWAN-UHUSIANO

China yatishia kuvunja uhusiano na Marekani kufuatia ziara ya rais wa Taiwan

Rais wa Taiwan, Tsai Ing Wen, katika mji wa Houston, Januari 7, 2016.
Rais wa Taiwan, Tsai Ing Wen, katika mji wa Houston, Januari 7, 2016. REUTERS/James Nielsen

Rais wa Taiwan Tsai Ing-Wen ameanza ziara ya siku 9 ambapo atazuru Honduras, Nicaragua, Guatemala na El Salvador. Nchi hizi zote zinatambua uhuru wa Taiwan ispokua China ambayo inadai kuwa Taiwan ni sehemu ya aridhi yake.

Matangazo ya kibiashara

China haifurahishwi na ziara hii, wakati ambapo rais wa Taiwan kwa kuzuru Amerika ya Kati alipitia nchini Marekani. Wiki chache tu zilizopita serikali ya China iliiomba Marekani kutomruhusu Weng Ing Tsai kuingia katika ardhi ya Marekani.

Beijing haikufurahishwa na rais Tsai Ing Wen kupitia nchini Marekani. Mkutano kati ya Rais wa Taiwan na Ted Cruz, mgombea wa zamani wa chama cha Republican katika kura za mchujo na seneta wa jimbo laTexas umethibitisha hofu ya China. "Tunapinga mkutano wowote kati ya kiongozi wa Taiwan na maafisa wa Marekani kwa kisingizio cha kupita tu nchini Marekani."

Tangu Desemba, mvutano kati ya China na utawala wa Trump umekua ukishika kasi. Kwa kukubali kupokea pongezi yaTsai Ing Wen kwa njia ya simu kwa kuchaguliwa kwake, Donald Trump alifutilia mbali hoja ya kuwa na "China moja."

Xi Jinping na rais mteule wa Marekani Donald Trump wakubaliana kukutana

Global Times, gazeti lililo karibu na chama cha kikomunisti nchini China kimeitishia Marekani. kama hii inaendelea, Beijing hali hii itaendelea China "italipiza kisasi" na "kuvunja mahusiano" yanayoiunganisha na Marekani.

Kabla ya kurejea Taiwan, Tsai Ing Wen atapita kwa mara nyingine tena nchini Marekani, itakuwa tarehe 13 Januari. Haijafahamika iwapo atakutana kwa mazungumzo na rais mteule wa Marekani Donald Trump, lakini katika mkutano wa hivi karibuni na vyombo vya habari, rais mteule wa Marekani aliwahakikishi viongozi wa China kuwa lazima wafute hoja ya kuwepo kwa China moja.