IRAN-USALAMA-AJALI

Watu wengi wapoteza maisha baada ya jengo kuporomoka mjini Tehran

Wazima moto walikua wametahadharisha juu ya hatari ya moto katika jengo la la ghorofa 15, ambalo lilikua lazamani katika mji wa Tehran.
Wazima moto walikua wametahadharisha juu ya hatari ya moto katika jengo la la ghorofa 15, ambalo lilikua lazamani katika mji wa Tehran. Tasnim News Agency/Handout via REUTERS

Zaidi ya Wazima moto 20 wamepoteza maisha Alhamisi hii Januari 19 katika baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 15 katikati mwa mji wa Tehran, nchini Iran, Meya wa mji huo amearifu.

Matangazo ya kibiashara

engo hilo lilikua na maduka mengi ya nguo na vifaa vya viwanda lilikua halikidhi viwango vya usalama.

Lilikua jengo la zamani la ghorofa 15 mjini Tehran. Lilijengwa katika miaka ya sitini. Siku ya Alhamisi, karibu saa mbili asubuhi, moto ulizuka kwenye ghorofa za juu. Wazima moto waliwasili mara moja katika eneo la tukio kuzima moto huo, mwandishi wa RFI katika mji wa Tehran, Siavosh Ghazi, amearifu.

Wazima moto 200 walikabiliana na moto huo kwenye jengo hilo la ghorofa 17 kwa saa kadhaa, kabla ya kuporomoka kwa sekunde chache.

Zaidi ya watu 200 pia nao waliripotiwa kujeruhiwa kwenye mkasa huo.

Jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1962, lilikuwa wakati mmoja jengo refu zaidi mjini Tehran.

Kwa mujibu wa kituo kimoja cha runinga cha serikali kilionukuu afisa mmoja, kati ya watu 50 na 100 wanaaminiwa kukwama chini ya vifusi.